Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa kitambulisho cha Marehemu 2Pac alichokitumia mwaka 1995 kitapigwa mnada na kampuni ya Memorabilia huku thamani ya kitambulisho hicho kikitajwa kufikia thamani ya shilingi Mil.4 za Kitanzania.
Inaelezwa kuwa 2Pac aliwahi kukaa jela miezi tisa baada ya kufunguliwa mashatka ya unyanyasaji wa kingono na ilimlazimu kubeba kitambulisho hicho kila aendapo, 2Pac alihukumiwa kifungo hicho April 14,1995 na kitambulisho hicho kilitolewa tarehe April 28,1995 kikiwa na saini yake huku kitambulisho hicho kikitajwa kutakwa na Wamarekani wengi.
Inaelezwa kuwa 2Pac alipokuwa gerezani aliwahi kuandika barua kwa mpenzi wake na alichora picha ya kimapenzi ikimuonyesha yeye pamoja mpenzi wake na kuelezwa kuwa barua hiyo iliuzwa kwa thamani ya zaidi shilingi Milioni 48 zaKitanzania na kampuni ya NSFW.
Rapper 2Pac Shakur alizaliwa June 16,1971 na kufariki September 13,1996 baada ya siku kadhaa kupita baada ya kupigwa risasi akiwa anaendesha gari mjini Las Vegas Marekani.
VIDEO: UMEPITWA NA HII YA MISS KINONDONI 2019 “HATUANGALII UZURI, TUNAANGALIA HESHIMA”? BONYEZA PLAY HAPA CHINI