Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

MO kaongea kama kuna timu inataka kumtoa Chama na Kagere Simba SC

on

Muwekezaji wa club ya Simba SC Mohamed Dewji ‘MO’ amekanusha mpango wa wachezaji wao Clotous Chama na Kagere kuwa wanaweza wakaondoka baada ya kudaiwa kuhitajika na timu vigogo Afrika, ambavyo vimewaona na kuvutiwa na huduma za wachezaji hao.

MO Dewji ameeleza kwa sasa kuwa wanajenga timu hivyo sio rahisi kwa wao kukubali waachie wachezaji wao muhimu kama Chama na Kagere waondoke, kwani hiyo ityakuwa ni kinyume na malengo yao ya kutaka kufika mbali zaidi.

Habari za Cloutous Chama na Kagere kuhitajika na timu nyingine nje ya Simba SC hiyo sio kweli sababu, MO Dewji amethibitisha kuwa na mikataba na wachezaji hao, au kama timu itakayowahitaji basi watoe pesa ya juu sana itakayowafanya wamudu kusajili wachezaji bora wengine.

Ukimuuliza Mwinyi Zahera ishu za Ajib kurudi Simba SC….

Soma na hizi

Tupia Comments