Inadaiwa kuwa hii ndio video ambayo inamuonesha mtu ambaye anadaiwa kuwa ni rapper J.Cole akivamiwa na kupigwa ngumi akiwa nchini Nigeria alipokwenda kutumbuiza kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mtoto wa bilionea nchini humo.
Baada ya stori hizo kuenea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa J Cole hakuumia sana ingawa alipigwa ngumi nyingi na kuibiwa baadhi ya vitu vyake , sasa meneja wa J Cole amejitokeza na kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa mtu yule sio J Cole kama watu walivyokuwa wakidhania.
“Wengi wenu inabidi muache kunitaja kuhusu hii video ya Cole na huyo mtu wanaefanana nae kupigwa ngumi, mimi pia ilinibidi niangalie mara mbili baada ya kuiona hiyo video kwa mara ya kwanza. Cole anafanana na wengi duniani hapa”>>> Ibrahim Hamad, meneja wa Cole na mwanzilishi mwenza wa Dreamville Records.
ULIPITWA NA USHINDI WA TAIFA STARS/ RUBY KUPATA MTOTO/ FLAVIANA NA RIHANNA? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUATAZAMA MWANZO MWISHO