Golikipa mahiri wa zamani wa klabu ya Simba Juma Kaseja ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya, bado ana historia nzuri na kubwa ndani ya klabu ya Simba, kwani ni miongoni mwa magolikipa mahiri waliowahi kuidakia timu hiyo kwa mafanikio.
Kama ambavyo wengi hufahamu mtu akifanya vizuri ni lazima apongezwe Juma Kaseja usiku wa February 1 kupitia account yake ya instagram ameandika ujumbe ambao kwa mara moja ni ngumu kuelewa kamaanisha nini, Kaseja katika account yake ya instagram kaandika “Wana ssc nikumbukeni kwa mabaya nilio wafanyia kwenye timu yenu mazuri yaacheni”
Hizi ni comment za mashabiki
- kajolejrMm bro sijakuelewa kabisa… Sisi wana simba bado tunakukukubali kwa yote make ndo mpira na tunaamini one day utakua kwenye bench la ufundi la msimbazi kama head coach au assistant coach au goalkeeper coach@official_juma_kaseja
- dogolechaUna mana gani@official_juma_kaseja
- erickwanguDaaaaaaaah maneno yameniuma sana kaka…ila weee ndo namba moja yetu eva en eva trust ilo kaka… @official_juma_kaseja@official_juma_kaseja
- iam_manotautdUmekumbuka nini juma? Maneno mazito hayo unayoongea ila kifupi wewe upo katika makipa wenye historia katika chama la wekundu
- mohamediramadhani01Sidhani kma kuna mwana msimbaz Wa kkuchukia wwe na kma yupo bas hajielewi.@official_juma_kaseja
- kiyogomajailosKwnini umesema ivyo juma k juma nainyimba ilikua atali
- mwasiamaniwana simba daima tunakukumbuka juma k juma.
- omaryomary86Tunakukumbuka kwa Mazuri bro always your in my heart
- sweerbertHakika atakae kusema wewe vibaya ndani ya simba ataanza kulaaniwa yy coz wewe ulikua na mchango mkubwa sanaa kwenye timu…
- ashuraomaryTunkkmbuk kW mazur tu
Inashangaza kidogo Juma Kaseja kamaanisha ni kuandika hivyo, kwani utamaduni wa wengi ni mtu huwa anakumbukwa kwa mazuri na sio mabaya.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.