Rais Magufuli ametoa salamu za pole kwa walioguswa na msiba wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani DW, Isack Gamba.
Akitoa salamu za Rais Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili Isack katika viwanja vya Lugalo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu Gerson Msigwa amesema Rais Magufuli ameguswa na msiba huo.
Msigwa amesema “kwa niaba ya Rais napenda kutoa pole kwa familia ya Isack Gamba, na wote ambao mmekusanyika hapa, niseme tu mheshimiwa Rais anawapa pole sana na amesema anatupenda na anafuatilia kazi zetu na kazi kubwa tunazofanya kwenye kutimiza malengo ya nchi.”
“Alitamani sana kuwepo kwenye msiba wa Isack Gamba lakini bahati mbaya majukumu yamembana ameshindwa kuja na anamwombea heri Mungu amlaze mahali pema peponi”, Msigwa.