Mshambulizi chipukizi Samuel Mbangula na mlinda mlango Carlo Pinsoglio wameandikisha mkataba mpya kwenye klabu ya Juventus
Mbelgiji Mbangula, 20, ameongeza mkataba wa miaka miwili na kupeleka makubaliano yake hadi 2028.
Wakati huo huo, kipa Pinsoglio mwenye umri wa miaka 34 ametia saini mkataba wa 2026.
Mkataba wake wa awali ulitarajiwa kuisha mwezi Juni.
Pinsoglio akitia saini kandarasi mpya itakayodumu hadi msimu wa joto wa 2026 na baada ya kusaini mkataba huo mpya, alituma ujumbe kwa mashabiki katika video iliyowekwa kwenye akaunti ya X ya klabu:
“Mashabiki wa Juventus, nina furaha sana kusaini mwaka mwingine na familia hii nzuri, Forza Juventus.”