Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kufungwa katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi C hatua ya michuano ya African Cup of Nations dhidi ya Senegal, mastaa mbalimbali Tanzania wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kusikitika kuhusiana na kipigo cha 2-0.
“Huyu kambale straika teleza angekuwepo je?acheni nyie..tumshukuru Mungu kwa yote”>>> Mwana FA
“Tumecheza vizuri kuliko msimu uliopita ila possession 39% is very sad na coordination kidogo sio poa inanifanya nihisi hakuna set pieces. Manula na Ramadhani wameteseka balaa. All in all it was a good game but we lost. Tupige supu ya pweza tunawaua next game. Tukumbuke tuliocheza nao wapo rank ipi bandugu. Nipo very positive kwa jinsi naiamini team yangu. We are going through 💪🏽 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🙌🏽🙌🏽🙌🏽”>>> Idris Sultan
“Nilivyokuona tu nilikujua Mapema Sana Kama una roho Mbaya, Alafu utasikia siku linataka kuja Tanzania kwenye Mbuga zetu kutalii jaribu uone Kama hatujakusakizia SIMBA wakutafune, Kwani ungepiga Kishutu cha kawaida ungefukuzwa Kwenu ..?? Sasa Kama ulikuwa ujui lengo la Hili Kombe ni kujenga Mahusiano Mazuri kati ya TANZNIA na SENAGAL Kwa ujinga wako na sifa zilivyokujaa umevunja Mahusiano Mwehu Wewe ….sifa zitakuuwa”>>> Mkude Simba
“MANULA MWENYEWE KAMUOGOPA!!🏃🏾♂️ #StazTunahitajiMtuWaKufanyaCastingTupateSuraHiziKikosiniMwanawaneee#
#DahHuyuJamaaaKamaIsingekuwaBoliiiiSijuiAngepigaDealGaniLabdaJeshiniKikosiCha……FillInTheBlanks😂#”>>>Mkandamizaji
“Da uyu mkatili ona rangi anazo zipenda angalia simu angalia ndula katili”>>> Mkubwa Fella
“Tumefungwa 2 kwa tabu sana. Refa hakuwa wetu,ndo maana soka la Afrika haliendelei figisu kubao. Tumewazidi Senegal kwa kila kitu tumeonesha kwamba hawatuwezi, Tutawapiga Kenya Na Algeria maana uwezo wetu ni mkubwa mno tutasonga mbele. MZALENDO HALISIA HAPA”>>> Nashe Mcee
VIDEO: Okwi baada ya kukabidhiwa tuzo AFCON 2019