AyoTV

“Acheni tamaduni za zamani, pelekeni watoto shule” – Mwigulu

on

Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jamii ya kifugaji Jimboni kwake kuacha tamaduni zao za kutowapeleka watoto shule na kuwatumikisha kuchunga mifugo yao.

Waziri Mwigulu amezitaka jamii hizo kuacha utamaduni huo kwa kuwa sasa hali ya maisha imebadilika tofauti na miaka 20 iliyopita ambapo kulikuwa na sehemu kubwa ya kufugia mifugo yao lakini sasa mabadiliko ya hali ya hewa ni tofauti sana kwa sababu ya ukame hivyo kuwekeza katika watoto kusoma kutawasaidia baadaye wazazi hao.

Soma na hizi

Tupia Comments