Zitto Kabwe ni mbunge wa Kigoma mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo ambaye amekuwa akiziandika headline mbalimbali kupitia uwezo wake wa kuichambua siasa, leo September 19 2016 Zitto kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika ujumbe huu.
‘Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL? Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi Bilioni 300 na riba. Kiwango Hicho Ni zaidi ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda‘ -Zitto Kabwe
‘TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais Kwanini hashughulikii Ufisadi huu wa IPTL/PAP? Nini Kinamzuia Rais Kuchukua Hatua dhidi ya Wizi huu wa Dhahiri Kwa Taifa?‘ –Zitto Kabwe
‘Tanzania Tunapata Hasara mno, Na Hizi zote Ni Fedha za Wananchi zitakazopotea‘
• ‘Watanzania mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye “TEGETA escrow account”, Fedha ambazo ziligaiwa Kwa Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri‘ –Zitto Kabwe
• ‘Watanzania Mmewapa Mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa “capacity charges” mpaka sasa – Kinyume Kabisa na Maazimio ya Bunge yanayotaka Mitambo Husika itaifishwe‘ –Zitto Kabwe
• ‘Baada ya Hukumu hii Watanzania tutawalipa Standard Chartered Fedha zao kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo (Kama tungelazimika Kulipa) tungezitoa kwenye Akaunti ya Escrow – Lakini sasa tutazitoa Hazina zikiwa ni Kodi za Watanzania‘ –Zitto Kabwe
Ushauri Wangu – Rais achukue Hatua Zifuatazo:
• Awafikishe Mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow.
• Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO (Kama ilivyoazimiwa Na Bunge).
• Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha Mahakamani Kwa makosa ya Utapeli, Wizi, Uhujumu Uchumi, Utakatishaji wa Fedha nk.
• Ahakikishe Taifa halilipi Fedha Hizi Kwa Standard Chartered. Benki iliyotumika Kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni tunalotakiwa kulipa.
MUHIMU: Rais AAMUE Kusimama na WATANZANIA au kusimama na “Matapeli wa TEGETA escrow“.
ULIMIS ALICHOZUNGUMZA ZITTO KABWE KUHUSU KONGAMANO LA BAJETI