Taarifa ninayokusogezea ni ya David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, tunafahamu ana kesi Mahakamani ya kupinga matokeo ya ubunge 2015 jimbo la Kigoma Kusini kesi ipo Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, taarifa ikufikie kuwa Kafulila baada ya kufika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma akasomewa kesi mpya ambayo anakiri hakuwa anaifahamu mwanzo kwenye sentensi zake; – David Kafulila
‘Nilifikishwa mahakamani kwa kesi mpya ukiachilia kesi ya kwanza ya kupinga matokeo ya uchaguzi 2015 jimbo la Kigoma kusini, awali nilikuwa nikijua ninakesi moja katika mahakama ya hakimu mkazi kigoma kwa madai kwamba nilimdhalilisha aliyekuwa mkuu wa wilaya Khadija Nyembo tangu mwaka 2013….nikiwa mahakamani nikapewa tena kesi nyingine ni kesi ya kuhamasisha wananchi wasichangie mchango wa maabara; – David Kafulila
‘Bado msimamo wagu utabaki palepale kwamba nitaendelea kupigania nchi yangu, kesi hizi zote katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma ukitazama hati za mashitaka yote ya Kafulila hapa Kigoma zimeandaliwa na kusainiwa na DPP makao makuu Dar es salam inawezekanaje;- Kafulila
Unaweza kubonyeza play kumsikiliza David Kafulila hapa
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.