Michezo

Gareth Bale kamkaribisha Zinedine Zidane kwa kuwafunga hat-trick Deportivo La Coruna (+Pichaz&Video)

on

January 9 ni siku ya mapumziko kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi, kwa sasa ni michuano mikubwa pekee kwa Tanzania inayoendelea, baada ya Ligi Kuu Tanzania bara kusimama ili kupisha michuano hiyo. Mtu wangu wa nguvu hiyo haimaanishi kuwa burudani ya soka ndio hiyo pekee.

1545

January 9 klabu ya Real Madrid ya Hispania ikiwa na kocha wake mpya Zinedine Zidane katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania chini ya kocha huyo, imeibuka na ushindi wa jumla ya goli 5-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu.

4248

Real Madrid wakiwa na kocha wao huyo mpya, walionekana kujitahidi kucheza mchezo wa kuvutia na kufanikiwa kuvuna point tatu muhimu  kwa magoli ya Karim Benzema dakika ya 15, 90 na kufuatiwa na hat-trick ya Gareth Bale kwa kufunga goli tatu dakika ya 23, 49 na 63. Huu ni ushindi ambao tunaweza sema umemkaribisha Zidane Santiago Bernabeu.

2048

Video ya magoli ya Real Madrid Vs Deportivo La Coruna

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments