Tukiwa tumemaliza headlines za Uchaguzi mkuu 2015, stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa msanii wa Hip Hop Kalapina ambaye alikuwa ni mgombea wa Ubunge jimbo la Kinondoni Dar es Salaam.
Novemba 4 2015 Kala Pina ameongea kuhusu ishu ya Uchaguzi Mkuu ulivyokuwa na kile ambacho hakikumridhisha kwenye mchakato wa kutangazwa matokeo ya Mbunge wa Kinondoni >>> ‘Kiukweli matokeo yale ya Jimbo la Kinondoni sikubaliano nayo kutokana na mapungufu ambayo yalikuwa yamejitokeza katika uchaguzi… kulikuwa na mapungufu mengi ikiwemo kutishwa kwa mawakala wangu katika kata ya Tandale kilichopelekea baadhi ya mawakala wangu kuondoka na wengi walikuwa akina mama‘ >>> Kala Pina.
‘Kulikuwa na mapungufu hata msimamizi msaidizi wakati anatangaza matokeo aliomba itumike busara kwamba kuna vituo takribani 19 havikuweza kujumlishwa katika matokeo ya kumtangaza mshindi hali hiyo mimi ninaona ni kukandamiza Demokrasia na kuwaminya wapiga kura zaidi ya elfu 30 ambao walikuwa nao wamefanya maamuzi ya kufanya kutafuta mwakilishi wao… wamenyimwa haki yao kwa hiyo wamenyimwa haki zao ikiwa vituo takribani 19 matokeo hayakujumlishwa‘ – Kala Pina
‘Nimeazimia kuupinga uchaguzi huu kwa kwenda Mahakamani kwa sababu naona Demokrasia haikutumika ipasavyo na iliminywa… kuna baadhi ya maeneo watu wanalalamika wamekimbilia Mahakamani kutokana na matokeo yasiyo sahihi, na mimi mwenyewe natarajia kwenda kusikiliza hii kesi Mahakamani wiki ijayo‘- Kala Pina.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE