Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Temeke, Elia Kakwembe, usiku wa kuamkia leo amesema licha ya kwamba wamefanikiwa kuzima moto uliozuka katika Kituo cha kuhifadhi mafuta cha Lake Oil, bado Timu maalum imeachwa katika eneo hilo ili kufanya uchunguzi wa kujua chanzo cha moto huo.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi na tutafanya uchunguzi wa kina kubaini nini chanzo cha moto kuanza na kuwaka kwa kasi sana, itatusaidia kupunguza majanga mengine ya namna hii, hakuna majeruhi waliopata majeraha makubwa” Kakwembe
ASKARI SHUJAA “ALIEJITOA MAISHA YAKE” KUZAMA KWENYE MATANKI MOTO UKIWAKA KUFUNGA VALVE