Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama Cha ADC, Queen Sendiga hii leo amefanya kampeni zake katika jiji la Tanga na kubainisha sera za Chama hicho ambazo zitatekelezwa iwapo Watanzania watampa ushindi kwenye kura za Urais kwenye uchaguzi wa October 28 2020.
Licha ya kunadi sera zake kwenye majukwaa lakini pia amepita kwenye Masoko ya mbalimbali kama soko la Mgandini, Ngamiani na Lango la Chumba ili kuongea na Wafanyabiashara juu ya yale atakayoyatekeleza huku kipaumbele chake kikiwa ni elimu Bure na kilimo.
Queen amesema “Tanzania tuna ardhi kubwa sana ambayo ikitumika ipasavyo itakuza uchumi wa Watanzania ikiwemo Wakulima kuwa na pesa, sera na vipaumbele vya Chama changu ni vitatu tu Elimu, Kilimo na Afya, Chama cha ADC tumekusudia kutengeneza na kuzalisha ajira zaidi ya milioni 10 katika miaka mitano ya mwanzo iwapo Watanzania watanichagua”