Kampuni ya Gazprom ambayo ni Msambazaji Mkuu wa gesi asilia nchini Urusi imesitisha usambazaji wa gesi kwa nchi za Bulgaria na Poland baada ya nchi hizo kukataa kulipia nishati hiyo kwa rubles.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano na kampuni hiyo imesema Sofia na Warsaw hawatapata huduma hadi watakapo tii masharti ya Moscow.
Kampuni hiyo imeonya kwamba ikiwa Bulgaria na Poland wataamua kutumia gesi inayosafirishwa kwenda nchi zingine, basi italazimika kupunguza kiwango hicho ambacho wataamua kuzuia kinyume cha sheria.