Mix

TOP 10: Zinazotajwa kuwa sehemu kali kwa ‘Honeymoon’ Afrika…Tanzania ipo?

on

Moja ya vitu vinavyochukua attention kubwa ya watu wanaotaka kuoana huwa ni sehemu nzuri kwa ajili ya FUNGATE yaani Honeymoon. Zipo sehemu nyingi mtu anaweza kuzitembelea lakini zipo hizi sehemu 10 zinazotajwa na Afrotourism kuwa nzuri zaidi kwa ajili ya Honeymoon barani Afrika kwa mwaka 2017.

10. Maporomoko ya Victoria – Zambia

Eneo hili ni la uoto wa asili lililoko katika Mto Zambezi na moja ya michezo maarufu eneo hili ni kucheza angani na kamba kwa kuning’inia maarufu kama ‘Bungee Jumping’, kusafiri kwa mitumbwi katika Mto huo na mengineyo.

9. Mbuga ya Maasai Mara – Kenya

Mbuga hii inasifika kwa wanyama wengi ikiwa ni pamoja na Nyumbu, Swala, Pundamilia na Paka ‘Nyau’ wakubwa na kufanya wale wanaopenda mandhari ya Mbuga kufurahia zaidi.

8.  Dioz – Tunisia

Eneo hili pia hujulikana kama ‘Lango la Sahara’, liko eneo la karibu na Beach, mbuga ya Jebil pamoja na Jangwa la Sahara eneo ambalo wanafungate hupenda kusafiri kwenda kwenye eneo la jengo hilo.

7.  Visiwa vya Tofo na Bazaruto – Msumbiji

Visiwa hivi vimetenganishwa kwa 247 km. Tofo hufahamika kama eneo bora zaidi kwa Utalii wa baharini barani Afrika wakati Bazaruto ina Mbuga ya wanyama ya baharini.

6. Hifadhi ya Asili ya Namib na Mbuga ya wanyama ya Etosha – Namibia

Maeneo haya mawili yanayopatikana Namibia yanasifika kwa muonekano mkubwa wa nyota nyakati za usiku, ambapo watu wengi hukodi vyumba visivyo na paa yaani ‘roof’ ili kufurahia muonekano huo.

5. Eneo la mapumziko katika Mlima wa Obudu – Nigeria

Eneo hili linasifika kwa kuwa na ‘Swimming pool’ ya asili, kucheza muziki, na kupanda Mlima huo.

4. Cape Winelands – Afrika Kusini

Eneo hili hujulikana kama Mji wa Mvinyo. Ni eneo maarufu na la kihistoria lenye shughuli za kusindika mvinyo au ‘Wine’. Watu wengi hupenda eneo hili kwani hujifunza mambo mengi kuhusiana na aina mbalimbali za wine.

3. Kisiwa cha Zanzibar – Tanzania

Watu wengi wa Afrika Mashariki wanakifahamu Kisiwa cha Zanzibar ambapo hupenda kutembelea hata kama haihusiani na harusi bali kufanya starehe na kupumzika.

2. Belo Sur Mer – Madagascar

Hapa ni maarufu sana kwa vivutio vya wanyamapori. Sur mer ni eneo ambalo lina shughuli za uvuvi lililo kimya na tulivu lililopo katika Pwani ya Magharibi mwa Madagascar.

1. Kisiwa cha Praslin – Shelisheli

Shelisheli ni Kisiwa kilichoundwa na Visiwa vidogo vidogo 115 katika Bahari ya Hindi. Praslin ni moja kati ya Visiwa hivyo ambapo hupokea wageni wengi sana hususani kwa honeymoon. Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO liliwahi kukiita Kisiwa hiki “Real-life Garden of Eden” yaani “Maisha Halisi ya Bustani ya Eden.”

Soma na hizi

Tupia Comments