Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya, March 4 kupitia kwa kocha mkuu wa timu hiyo raia wa Malawi Kinnah Phiri amethibitisha kuwa golikipa wao namba moja Juma Kaseja, hatokuwepo katika kikosi kitakachokutana na Simba siku ya Jumapili ya March 6.
Kocha huyo amethibitisha kuwa Juma Kaseja ambaye pia amewahi kuichezea Simba kwa nyakati mbili tofauti, hatokuwepo kikosini kwa sababu ya kushughulikia matatizo ya kifamilia, hivyo bado hayajaisha na ameamua kumuongezea muda.
“Anaondoka Mbeya siku tano zilizopita tulikubaliana kuwa ataungana nasi hapa siku ya leo, nimezungumza nae leo asubuhi kuna mambo muhimu ya kifamilia amenieleza hivyo basi nimeamua kumuongezea siku kadhaa za kubaki nyumbani kushughulikia yale yote yaliyopo kwenye familia yake” >>> Kinnah Phiri
Juma Kaseja ambaye amefanikiwa kupata watoto mapacha hivi karibuni na mkewe Nasra, aliondoka Mbeya baada ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons uliyochezwa uwanja wa Sokoine.
CHANZO CHA STORI HII: mbeyacityfc.com
ULIYAKOSA MAGOLI YA SIMBA VS SINGIDA UNITED? TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE