Utafiti unaonesha katika watu 72,000 wanaopata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa mwaka, asilimia 40 ni vijana na kati yao asilimia 80 ni Wasichana wenye umri kati ya miaka 15-24.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Patrobas Katambi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau unaotekeleza afua za VVU na UKIMWI zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana.
Katambi amesema kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2016-2017 unaonesha katika watu 72,000 wanaopata maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa mwaka asilimia 40 ni vijana na kati ya hao asilimia 80 ni wasichana wenye umri kati ya miaka 15-24.
“Hii ina maana kuwa katika kundi la vijana 10 walioathirika wanawake ni nane hivyo sisi tukiwa kama vijana tunatakiwa kuliangalia jambo hili kwa umakini hali kwa wasichana sio nzuri,” Katambi
Pia, amesema kiwango cha ushamili kimeendelea kupungua sambamba na kiwango cha maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI.