Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepitisha viwango vipya kwa asilimia 118 ndani ya miaka minne huku wabunge wakilipongeza kutokana mabadiliko chanya ya uendeshaji wa Shirika hilo.
Akitoa maelezo ya Shirika wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Wabunge, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, alisema ndani ya miaka minne wamepitisha viwango vipya 1600 ambayo ni sawa na aslimia 118 kutoka kwenye lengo la kupitisha viwango 1,350.
Amesema pia wamepima sampuli zaidi ya 74,000 kati ya lengo la kupima sampuli 71,000 ikiwa ni asilimia 115. “ Tangu mwaka wa fedha 2016/2017 mpaka Desemba 2019 wametoa gawio serikalini la Sh bilioni 36.4 kwa mujibu wa sheria huku akibainisha kuimarisha na kufungua ofisi za kanda Aidha, alisema changamoto wanayoipata ni bidhaa zisizo na ubora kuingizwa nchini kwa njia za panya.
Aidha, wabunge wameonyesha kuridhishwa na mabadiliko chanya ya kiutendaji katika shirika hilo ambapo kila aliyechangia alitoa pongezi.
Akichangia Mbunge wa Viti maalumu, Gimbi Masaba (CHADEMA) amesema kumekuwapo na mabadiliko makubwa ya kiutendaji ya Shirika. “ TBS ya mwaka 2016, sio hii ya sasa, utendaji kazi wao umeimarika sana, mnynge mnyonegni haki yake mpeni, nawapongeza kweli.
“ Mimi nishahidi, nimekwenda TBS na sikuwa nimejitambulisha kama mimi ni mbunge, nilikwenda kama mwananchi mwingine, nilihudumiwa vizuri, wakikuambia njoo baada ya siku ya nne kuchukua majibu, unaenda na unayakuta.” Masaba
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Saddiq Murad (CCM), alisema pamoja na kuwa uanzishwaji wa utaratibu wa kuwahudumia wananchi kimtandano kuwa na mafanikio ni vyema wakaweka dawati maalumu ambalo litasaidia kuhudumia wale watu ambao wanataka kujieleza zaidi.
“ Najua kuanzisha huduma online (matandao) kumekuwa na manufaa makubwa, kwanza mmekuwa mkiwahuduma watu wengi kwa wakati mmoja, lakini pia limeonoa mianya ya kuwepo na rushwa pale wanapokutana” Murad
“ Lakini kutuma maombi na kujibiwa kumekataliwa hakitoshi, kuna watu wanatakiwa kujieleza ili umuelewe na kumsaidia kuliko kila kiti kumalizia kwenye mtandano, hivyo muweke dirisha la kama mtu hakuridhisha nay ale aliyojibiwa online basi afike kujieleza na ahudumiwe”
Naye Mbunge wa Bahi, Omary Badweli (CCM) aliishauri TBS kuhakikisha inaweka dirisha la shirika lake kwenye kila ofisi za halmashauri ili kuweza kusogeza huduma zaidi kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa kamati hiyo, aliagiza wizara kuhakikisha ifikapo Januri 24 mwaka huu inawasilisha taarifa ya utendaji ya TBS ili ijumuishwe kwenye taarifa ya mwisho ya kamati.
Naye Mbunge wa viti maalum, Josephine Genzabuke (CCM) aliipongeza TBS kwa kuanzisha ofisi Kigoma na kuishauri kuweka watumishi wengi ili waweze kudhibiti mipaka na uingiaji wabidhaa zisizo na ubora hasa kutokana na mkoa kupakana na nchi nyingi.
Semina hii kwa wabunge wa kamati ya Viwanda ,Biashara na Mazingira iliandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa nia ya kupanua uelewa kwa kamati hiyo juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.
WIZARA “HEKIMA ITATUMIKA USAJILI WA LAINI KWA WASIO NA VITAMBULISHO VYA TAIFA”