Ad

Mix

Kinachofatia ni hiki kwenye Chuo kilichofungwa Kenya baada ya shambulio la kigaidi..

on

Kuna vyuo vina majina makubwa Kenya kama Nairobi University, Kenya University.. jina la Garissa University lilifahamika na kusikika zaidi baada ya kutokea shambulio la kigaidi na kupelekea mauaji ya wanafunzi zaidi ya 140.

Ripoti nyingine kutoka Kenya imethibitisha kwamba Kikao kitakachofanyika ndani ya wiki mbili kuanzia leo kitaamua lini Chuo hicho kitafunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi nane.

William Ruto, Makamu wa Rais Kenya

William Ruto, Makamu wa Rais Kenya

Makamu wa Rais Kenya, William Ruto ameonana na baadhi ya viongozi wa eneo la Garissa, kaskazini mwa Kenya na kuwahakikishia kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya usalama inakuwa sawa kwenye maeneo hayo ambayo yamekuwa yakikumbwa na mashambulizi ya kigaidi mara nyingi.

Tukio la shambulio hilo ni moja ya matukio ambao yaliwaumiza sana Wakenya kwenye mwaka 2015.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments