Mfanyabiashara mwenye asili ya Uingereza Richard Alden amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Grace Wangechi Kinyanjui ambaye alikuwa ni mke wake wa pili katika nyumba yake ya kifahari nchini Kenya amefikishwa mahakamani baada ya polisi kukataa madai yake kuwa alijiua mwenyewe.
Mfanyabiashara huyo baada ya tukio alimpeleka Grace Wangechi Kinyanjui hospitalini akidai kajipiga risasi mwenyewe na Kinyanjui alifariki muda mfupi baadae kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata. Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na ataendelea kushikiliwa siku tano zaidi wakati polisi wakiendelea na uchunguzi.
Kamanda wa polisi Japheth Koome amesema wanandoa hao wamekuwa kwenye mahusiano na walikuwa wanaishi pamoja pia majeraha ya Kinyanjui yanaendana na mauaji na kulikuwa na jeraha la risasi nyuma ya kichwa chake pia alikuwa na majeraha matatu upande wa kushoto wa shingo yake.
ULIKOSA WALIYOYAZUNGUMZA CCM BAADA YA UPINZANI KUSEMA WANAENDA KWA WANANCHI KUSHITAKI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE