January 5 2016 niliisogeza kwako stori ya Wakenya iliyoweka headlines kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo watu wengi walianzisha mjadala wa kuwataka Watanzania wote wafungiwe matumizi ya Instagram kutokana na matumizi mabaya ya baadhi ya Watanzania! Lakini sio Wakenya wote wanakubaliana na #KickTanzaniansOutOfIG.
Hizi ni baadhi ya posts za @XtianDela Mkenya aliyeanzisha mjadala wa #KickTanzaniansOutOfIG…
>>> “#KickTanzaniansOutOfIG Maadili yangu hayawezi kuniruhusu kuendelea kuwafollow Watanzania. Naeelwa kwa dhati kabisa kuwa sio WATANZANIA WOTE hupost vitu vya utu uzima, lakini kutokana na kujichanganya kwetu na mahala tulipo tukizungumzia search ya Instagram Discover Page, utaletewa page chafu za Watanzania na kwakuwa wao ndio wenye umaarufu zaidi na wenye followers wengi zaidi, Instagram inakuletea zile pages zenye umaarufu mkubwa kwenye eneo ulilopo na watu unao-wafollow. Kwahiyo ukifollow MTANZANIA YEYOTE, Discover Page ya Instagram inakupa option ya ku-follow pia zile page za Watanzania zenye UCHAFU MKUBWA… Ni kwa sababu hiyo nimeamua KU-UNFOLLOW WATANZANIA WOTE kwenye Instagram isipokuwa tu wale ambao nina uhusiano wa karibu nao!” <<< @XtianDela.
>>> “ #KickTanzaniansOutOfIG Nyerere hakuiaga dunia kwa ajili ya haya! Nyerere hakuhangaika ili nyie mje kupost picha za utu uzima kila sehemu! Kuna watoto kwenye Instagram! Kueni na muanze kupost vya maana! Kama Waafrika tunahjitaji tusimame na tutokomeze huu ujinga na kuutupia mbali. Nasimama dhidi ya Tanzania na picha za utupu!! #UnfollowTanzanians!! #KickTanzaniansOutOfIG!!” <<< @XtianDela.
Na hizi ni baadhi ya posts za Wakenya wanaopinga #KickTanzaniansOutOfIG kwa kutumia hashtag ya #IStandWithTanzanians kwenye Instagram…
>>> “Watu wapo bussy kuwafukuza Watanzania kwenye Instagram, lakini hapo walipo hawana kodi ya nyumba. Mwenye nyumba atakuwa anakufukuzwa wewe kwenye nyumba yake…” <<< @kevin_bundi.
>>> “ Sipingi maoni ya mtu yeyote wala mitazamo lakini kuna uhuru kwenye mitandao ya kijamii, watu wanapost vitu vya ajabu na picha na videos za ajabu pia lakini hiyo haimaanishi ni ajabu kwa kila mtu… IG watu wanajiexpress watakavyo, Wakenya, Wabongo, Wanaija, Wazungu kwa Waarabu… kwahiyo kwenye hilo… #IStandWithTanzanians #IStandWithTanzanians.” <<< @izohgee.
>>> ” Mshangao wa @xtiandela pale #IStandWithTanzanians #RestInPeaceXtianDela hii sio vita yako, achia Mungu atawale hehehe” <<< @cyrokeep.
>>> “Mshangao wa Dela akiona Wakenya wakisupport Tanzania @Regrann from @lynne_mcdee – Hahahahahahaaa acha niachie hapo kwa leo ila hii kampeni yenu mmh ni no no kwangu sitaki beef na WaTz #IStandWithTanzanians…” <<< @kamenace.
>>> “#Regrann from @ditram_ @xtiandela…. unadhani Instagram ni ya babu yako! Boya wewe! #IStandWithTanzanians.” <<< @kenyan_teammafisi.
>>> “@XtianDela umeiangusha hii nchi…. #IStandWithTanzanians” <<< @iam_bett.
>>> “ Hahaha umaarufu kweli unabadilisha watu #hashtegi #KickTanzaniansOutOfIG #IStandWithTanzanians #HapaKaziTu. Kwa bahati mbaya wanaunda 60% ya followers wako” <<< @briangau.
>>> “ Mtu ana followers 100+ anaona IG ni ya nyanya yake… Rafiki yangu Instagram haina muda wa kuwatoa WaTz . Ni rahisi sana Block ama Unfollow na sio kuchochea hapa vitu vya kijinga. Kuna wakati nawaza kweli unafikiriaje. Yani hiyo ndio akili iliyopata tuzo ya ‘the most sijui Twirra personality’ Dafaq, kivipi sasa? Kwa East Africa wao ndio wanaokimbiza IG, fanya yako @xtiandela.” <<< @lesley_daphney.
>>> “Maninja wanawachukia Watanzania na hapo wana uzito wa 5GB za ngono kwenye simu zao… Siwezi wachukia watu wenye sexy imagination” <<< @duncanisabwa.
>>> “@xtiandela akianzisha #KickTanzaniaOutOfIG dhidi ya vile alivyo log out IG after kuona #IStandWithTanzanians…. Naiachia hapa @xtiandela #IStandWithTanzanians” <<< @joementthairu.
>>> ” Yamesemwa yote!! #IStandWithTanzanians…“<<< @antoacedup.
>>> ” Nini shida na huyu @xtiandela ati #KickTanzaniansOutOfIG kivipi au hiyo itatokea lini, Instagram sio ya mtu hapa… wakati mnadiscuss #KickTanzaniansOutOfIG na post zenu za vituko, wenyewe wapo bussy kujenga uchumi wao na kuwapita Kenya… Chochote wanachopost Watanzania hakikuhsu.. kama hupendi Uwa-unfollow mbona sio kazi kubwa…. “@rashousmane.
>>> “ Kwa sababu tu yai moja limeoza kwenye tenga haimanishi mayai yote yameoza… “<<< @hesbonmberia.
>>> “ #IStandWithTanzanians… “<<< @Kevin_bundi.
>>> “ Watu turudi bustani ya Aden tukakae uchi. Nguo zimepanda bei… @tz.. instagram hawatutaki #IStandWithTanzanians.“<<< @csantos_07.
Kama una chochote cha kusema au kuongeza juu ya hili, share na mimi hapa chini kwenye comment.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE