Shahidi wa 12 upande wa Jamhuri Luteni Denis Urio katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu amekataa kuwa aliwahi kukamatwa na kuhojiwa katika kituo chochote cha Polisi licha ya washtakiwa kudai waliwahi kumuona.