Top Stories

Wahamiaji Haramu 77 wahukumiwa Mwaka Mmoja Gerezani

on

Leo February 23, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Wahamiaji haramu 77 kutoka nchini Ethiopia jela mwaka mmoja baada ya kukiri makosa ya kuingia na kuishi nchi kinyume na sheria.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ambapo amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa baada ya kukiri makosa yao.

Hakimu Mwambapa amesema kuwa kutokana na washtakiwa kukiri makosa yao anawahukumu kwenda jela mwaka mmoja ama kulipa faini ya Shilingi Milioni 1 kwa kila mshtakiwa.

Hata hivyo, wahamiaji hao wameshindwa kulipa faini hiyo, ambapo wamepelekwa gerezani kwa ajili ya kutumikia hukumu hiyo.

Kwa pamoja raia hao wanadaiwa February 8,2018 walikutwa wameingia nchini kinyume na sheria maeneo ya Kigamboni Dar es Salaam bila kuwa na hati ya kusafiria (Passport) wala nyaraka za kuonyesha uhalali wao wa kuwepo nchini.

Pia wanadaiwa katika tarehe hiyo ya February 8, walikutwa maeneo ya Kigamboni DSM wakiishi kinyume na sheria bila kuwa na kibali chochote cha kuonyesha uhalali wao.

KAULI YA CHADEMA ARUSHA BAADA YA MADIWANI WAWILI KUHAMIA CCM.

Soma na hizi

Tupia Comments