Idadi ya Majambazi waliouawa na Polisi wakati wa jaribio la uporaji wa kutumia silaha katika Mtaa wa Kanyamahela Mjini Kibondo imeongezeka kutoka watatu hadi kufikia sita mara baada ya Jeshi la Polisi Kigoma kuwaua wengine waliofanikiwa kukimbia wakati wa mapambano makali kati yao na Polisi usiku wa March 30 mwaka huu.
Akizungumza ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Martin Otieno amesema baada ya majambazi hao kukimbia kusikojulikana Jeshi hilo liliendelea na operesheni ya kuwasaka na kufanikiwa kupata taarifa kutoka kwa Wananchi baada ya kuonekana wakielekea katika kambi ya wakimbizi ya Nduta.