Leo October 5, 2018 Mahakama Kuu mjini Kigali imeamua kumuachilia huru kwa dhamana mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara na mamake na watafuatiliwa wakiwa nje ya gereza.
Jaji wa mahakama kuu mjini Kigali ametangaza kwamba maombi yao ya dhamana yamekubaliwa lakini wakawekewa masharti ya kukabidhi Pasport zao kwa mwendesha mashtaka. Aidha wametakiwa kutovuka mipaka ya jiji la Kigali bila kibali maalumu.
Wawili hao walikuwa kizuizini tangu mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. Walikanusha madai hayo wakisema yana misingi ya kisiasa.
Mashtaka yanayomkabili Rwigara na mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati aliamua kuwania urais.