Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Wachezaji wa Barcelona wamemgeukia kocha wao kutolewa Champions League

on

Wachezaji wa FC Barcelona ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka waondolewe katika michuano ya UEFA Champions League wamemgeukia kocha wao Ernesto Valverde, hiyo ni kwa mujibu wa stori  zinazoendelea kusambaa nchini Hispania.

Barcelona mchezo wa kwanza wa Champions League nyumbani kwao dhidi ya AS Roma walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-1 lakini mchezo wa marudiano waliruhusu kufungwa kwa magoli 3-0, hivyo wametolewa kwa goli la ugenini baada ya agg kuwa sawa ya magoli 4-4.

Ernesto Valverde

Baada ya kutolewa zimeripotiwa taarifa kuwa wachezaji wa Barcelona wanamlaumu chini chini kocha wao Valderde kuwa kabla ya kurudiana na AS Roma walimshauri kuwa huu ni mchezo ambao wangepaswa awaandae kucheza kwa kutumia nguvu zaidi ili kukabiliana na Roma ila hakutilia maanani ushauri huo.

Ushauri huo inadaiwa kuwa Valderde aliuchukulia poa na kufanya mabadiliko ya mbinu kwa uchache tu kitu ambacho kilimpa uhuru zaidi wa Edin Dzeko kufanya vizuri dhidi ya Barcelona  lakini kabla ya game walimwambia “Boss huu ni mchezo wa kutumia nguvu” kocha wao aliwasikiliza lakini hakutoa jibu la moja kwa moja.

ALL GOALS: Simba vs Mbeya City April 12 2018, Full Time 3-1

Soma na hizi

Tupia Comments