Kocha wa zamani wa Club ya Arsenal aliyewahi kudumu na club hiyo kwa miaka 22 Arsene Wenger ameamshauri kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane kuwa kama anataka kuwa kocha katika kiwango cha juu ni lazima aende kufundisha soka nchini England akiwa hajataja club anayomshauri ajiunge nayo.
Zidane toka aachene na Real Madrid mwezi May bado hajaajiliwa na club yoyote ile zaidi ya kutaka kupumzika lakini amekuwa akihusishwa kuwa mbioni kujiunga na club ya Man United inayofundishwa na kocha Jose Mourinho ila imekuwa haina matokeo mazuri kwa hivi karibuni.
“England ndio nchi pekee ambayo kuna club sita ambazo zote zina uwezo wa kuwania Ubingwa, kwa nchi zote mwezi December unaweza ukajua kabisa kimsingi ni timu gani inaenda kutwa Ubingwa wa Ligi Kuu lakini sio England, Ufaransa mwezi September tu unajua timu gani itakuwa Bingwa wa Ligi”>>>Arsene Wenger
Kauli ya Wenger imetoka na kuashiria kuwa Zidane kama ataenda England ndio sehemu atakayopata changamoto lakini Ligi nyingine hakuna ushindani na rahisi kutabiri Bingwa atakuwa nani mapema tu, Zidane aliondoka Real Madrid mwezi May baada ya kuweka rekodi ya kuingoza Real Madrid kutwaa UEFA Champions League mara tatu mfululizo.
MO Dewji alivyojitokeza Taifa kwa mara ya kwanza baada ya siku 49 toka atekwe