Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limetangaza rasmi kupokea taarifa za rufaa ya club ya Chelsea ya England, ambayo hivi karibuni ilikumbana na adhabu ya kufungiwa kwa madirisha mawili kutokufanya usajili wa mchezaji yoyote.
Chelsea walipewa adhabu ya kutofanya usajili wa mchezaji yoyote baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na kudaiwa kuwa walimsajili staa wa Burkinafaso Bertrand Traore akiwa na miaka 16 mwaka 2017, kitu ambacho ni kinyume na sheria na kanuni za FIFA.
Baada ya kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo FIFA imepanga kusikiliza shauri la Chelsea April 11 ili kutoa uamuzi wa mwisho, adhabu waliyopewa Chelsea iliambatana na faini ya pound 460000 huku FA pia wakipigwa faini ya pound 390000.
MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS