Takribani saa na moja na nusu kabla ya klabu ya Manchester United na Arsenal kuumana katika mchezo wa ligi kuu ya England, millardayo.com inakuletea taarifa za kuihusu klabu ya Man United ambayo inaenda kwenye mchezo huo ikiwa ndio timu inayoongoza kwa kuwa na wachezaji majeruhi.
Radamel Falcao, Ashley Young, Marcos Rojo, Daley Blind, Rafael, Jones, Micheal Carrick ni kundi la wachezaji tegemeo wa Manchester United ambao wanaweza kukosekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Gunners.
Wachezaji hawa wawe wazima au wameumia, kila wiki hulipwa mishahara yao kama ambavyo walikubaliana kwenye mikataba yao na klabu hiyo.
Kwa wikii hii tu Manchester United italipa kiasi cha £785,000 – zaidi ya billioni 2 za kitanzania kuwalipa mishahara wachezaji hao waliotajwa hapo juu.
Mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri sana na bado wapo majeruhi ni mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao, huku Van Gaal akithibitisha kwamba mshambuliaji huyo atakuwa nje ya uwanja wa wiki mbili baada ya kupata majeruhi kwenye misuli.
Falcao, ambaye yupo United kwa mkopo kutoka Monaco, anavuna kiasi cha £280,000 kwa wiki – kwa maana hiyo mshambuliaji tangu awasili Old Trafford ameshavuna kiasi cha £4m huku amecheza mechi 5 tu, akitoa assists mbili na kufunga goli moja.
Daley Blind atakuwa nje kwa miezi kadhaa baada ya kuumia goti, lakini mchezaji huyo bado atakuwa akivuta kiasi cha £75,000 kila wiki.
Mlinzi Marcos Rojo, ambaye analipwa £70,000 kwa wiki nae ameumia bega katika mchezo dhidi ya Manchester City. Atakuwa nje kwa wiki kadhaa zijazo.
Rafael, anayevuna £50,000 kwa wiki, ana tatizo la misuli, Jones (£50,000-a-week) nae yupo nje kwa wiki kadhaa sasa, wakati Evans (£65,000-a-week) ana majeruhi ya enka.
Katika safu ya kiungo, Ashley Young, ambaye hupeleka nyumbani kila wiki mshahara wa £115,000 ana maumivu ya groin lakini anategemea kurudi dimbani hivi karibuni.
Michael Carrick, ambaye anavuna £80,000 kwa wiki, alipata majeruhi ya misuli wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya