Kila siku duniani kunafunguliwa Hoteli na sehemu za starehe zenye utofauti wa kipekee ambapo leo zimenifikia hizi Hotel tisa zilizotajwa kuwa na muonekano wa kipekee na mzuri zaidi na zikiwa zimejengwa ndani au juu ya bahari kwa mujibu wa CNN
Inawezekana kabisa kwa muonekano huu wapo ambao wataogopa kuchukua vyumba vya chini ya bahari lakini wamiliki wa hotel hizi wanasema huna haja ya kuwa na wasiwasi maana vioo vilivyotumika kwenye madirisha ni vigumu kwa kiasi cha kugongwa na kitu kizito mpaka kilo 150 na kisivunjike.
Taj Lake Palace, Udaipur, India
Good Hotel London, Uingereza
Conrad Maldives
Salt & Sill, Sweden
Beach Villa Ocean Suites at Resorts World Sentosa, Singapore
Inakadiriwa kuwa kuna zaidi ya aina 50,000 za viumbe wa baharini huonekana kwenye vyumba vya chini ya bahari huku kukiwa na huduma ya internet ya Wi-Fi bure kwa saa 24.
Salt & Water Catamarans, Serbia
Salt & Water hufahamika pia kama nyumba meli kwa jinsi ilivyojengwa, bado ujenzi unaendelea ingawa inatarajiwa kukamilika mwaka huu ambapo kila chumba kitakuwa kinajitegemea kwa kila kitu kuanzia sehemu ya mapokezi na sehemu ya vinywaji.
OFF Paris Seine, Ufaransa
OFF Paris Seine’s Sunset Suite: Ina muonekano mzuri kwa ndani ikiwa imewekewa fanicha za kisasa ambapo Hotel hii ina jumla ya vyumba 54 vya kulala ambapo kuna huduma ya chakula na vinywaji kwenye kila chumba.
Solent Forts, Uingereza
Solent Forts: Majengo yake yalijengwa karne ya 19 na yalitumika kama ngome ya majeshi ya Ufaransa wakati wa vita kuu ya pili ya duniani kabla ya kutelekezwa mwaka 1960 yalipobadilishwa kuwa hotel, kuna vyumba vya kulala zaidi ya 30.