Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa ripoti ya mwenendo wa ugonjwa wa Kipindupindu nchini kwa mwezi wa February 2016
Akiongea na Waandishi wa Habari Dar es salaam, Naibu Waziri Dk. Hamisi Kigwangalla amesema ‘Takwimu za wiki iliyopita zinaonyesha kuwa kuanzia tarehe 22 hadi 28 ya mwezi Februari 2016, idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 473, na kati yao watu 9 walipoteza maisha.‘
‘Jumla ya Mikoa 12 nchini iliripoti wagonjwa katika kipindi cha juma moja lililopita ambapo Mkoa wa Mara uliripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa ambao ni 125, Iringa 64, Mwanza 59, Morogoro 44, Mbeya 29, Dar es salaam 25, Arusha 18, Kigoma 8, Rukwa 6, Simiyu 6 na Singida 2‘
‘Wizara inaendelea kutoa rai kwa jamii, Wataalamu na viongozi katika ngazi zote kwamba kila mmoja wetu atimize wajibu wake katika harakati za kuudhibiti ugonjwa wa Kipindupindu‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE