Unaweza ukadhani hakuna kingine kipya kuhusu maisha ya staa Kim Kardashian wa reality show ya ‘Keep Up with Kardashians’.
Upande wa maisha ya nyuma ya uhusiano wa Kim Kadarshian kabla ya kufunga ndoa na Kanye West, miongoni mwa wanaume aliowahi kuwa nao mapenzini ni pamoja na RJ, Reggie Bush, Kris Humphrie, Cristiano Ronaldo.
Lakini Kim Kardashian amesema kingine ambacho huenda hukuwahi kufahamu kuhusu uhusiano wake ya kwanza kabisa, aliingia mapenzini na mtoto wa kaka wa Michael Jackson aitwaye Tito Joe Jackson au TJ akiwa na miaka 14 tu.
Katika kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake kilichoandaliwa na Sean Smith kiliweka wazi uhusiano huo ambao hata hivyo haukudumu kwa muda mrefu na kuanza kutoka na RJ.
“Nilianza uhusiano nikiwa na miaka 14 tu” Kim…hakusita pia kumshirikisha mama yake mzazi Kris Jenner.
Msikilize hapa akiwa kwenye mahojiano..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.