Ad

Top Stories

PICHA 7: Rais Magufuli alivyomuapisha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, IKULU DSM

on

LEO January 18, 2017 IKULU Dar es salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemuapisha Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania.

Hafla ya kuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waheshimiwa Majaji wa

Mahakama ya Rufaa na Mahakama ya Kuu na Viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria. Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma amechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa.

Nimekuwekea hapa picha za tukio la kuapishwa kwa Jaji Ibrahim Hamis Juma

VIDEO: Ulipitwa na hii ya Rais Magufuli alivyocheka wakati kuwaapisha viongozi IKULU? Nimekuwekea hapa chini.

Soma na hizi

Tupia Comments