Moja ya habari iliyoandikwa leo January 8, 2017 ni pamoja na hii ya gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Kinadada wacharuka ulaji supu ya Pweza’
#NIPASHE Imeelezwa kuwa idadi ya wanawake wanakula Pweza inaongezeka kwa kasi na kuwazidi wanaume, kila kwenye wateja 10, wanne ni wanawake pic.twitter.com/Ea9d9pHrfM
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
Baada ya wanaume kusifika kuwa ndio walaji wakubwa wa minofu ya samaki aina ya Pweza na supu yake, hali sasa imebadilika baada ya kinadada kuonekana pia wakichangamkia kwa wingi kitoweo hicho kinachotajwa kuwa na sifa za kipekee kwa mujibu wa watumiaji.
Inaelezwa kwa wastani kupitia wauzaji waliozungumza na Nipashe imebainika kuwa kuna ongezeko la takribani asilimia 40 ya wateja wanawake anbayo ni karibu kila kwenye wateja 10 wanaoununua vipande vya Pweza au supu yake kuwa wanne ni wanawake.
Wanaume ndiyo walikuwa wakisifika kwa ulaji wa supu ya Pweza uliopamba moto jijini Dar es salaam katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo taarifa kwamba husaidia mambo mengi mwilini hasa katika kuimarisha urijali kwa wanaume.
UTAFITI WA KITABIBU:
Dr. Damas Mahenda ambaye ni Mhadhiri Msaidizi kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) amesema ni kweli samaki jamii ya Pweza wanafaida nyingi mwilini hivyo si ajabu kusikia watu wakichangamkia matumizi yake wakiwemo akina mama.
Dr. Mahenda amesema Pweza wamejawa na virutubisho vinavyosaidia mengi ikiwemo kuongeza hamu na kuboresha tendo la ndoa huku minofu yake ikiwa virutubishpo vya kumuwezesha mwanamke kuwa na sifa halisi za “Ukike” na pia mwanaume kuimarika afya yake.
Unaweza kuzipitia hapa chini habari zingine kubwa za magazeti ya leo January 7 2017
#MWANANCHI Mbinu za kuwashinda majambazi
1. Usitembee na fedha nyingi
2. Usitaje mipango yako
3. Umakini ATM
4. Usimuani kika mtu pic.twitter.com/gSvKvfNwHe— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#JAMBOLEO Madereva wamelitaka Jeshi la Polisi kutowekeza nguvu nyingi ktk kukusanya mapato kwa wakosaji badala yake watoe elimu ya usalama pic.twitter.com/NWMWbdZwYb
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#JAMBOLEO Serikali imekiri kuwa ina kazi ya kufanya ili kukomesha matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana nchini na vita hiyo ni ngumu pic.twitter.com/XLctUVDAsi
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#JamboLEO Ekisa Vuma mkazi wa Kigoma amejifungua watoto wanne ktk Hospitali ya Rufaa ya Mawenu kwa upasuaji, watoto wote wako salama kiafya pic.twitter.com/8NodPDt4aE
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#LETERAHA Pamoja na kipigo cha goli 4-0 dhidi ya Azam, timu ya Yanga wamesema wao wameshafuzu nusu fainali, wanaitaka uwanjani Club ya Simba pic.twitter.com/jki6nj68Lu
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#MWANANCHI Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayotokea duniani hayawezi kuzuiliwa na mifumo iliyopo pic.twitter.com/krmYUqt1C1
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#JAMBILEO Japo amestaafu, Rais wa awamu ya 4 Jakaya Kikwete ameendelea kukumbukwa na jamii hasa ktk mitandao, tofauti na kauli za upinzani. pic.twitter.com/VYdmPcgHwO
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#TANZANIADAIMA Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amesema CCM ina baadhi ya watu wenye roho mbaya kiasi cha kumwombea kifo na haikutimia pic.twitter.com/Hu6eVyEccs
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
#MWANANCHI Watu 31 waliokuwa wafanyakazi BOT bado wanaendelea kukumbwa na danadana za kisheria baada ya BOT kutoa ombi la kesi kupitiwa upya pic.twitter.com/QfsEB9zVdy
— millardayo (@millardayo) January 8, 2017
VIDEO: AyoTVMAGAZETI: Mtifuano mpya wa CCM, UKAWA, Kina Dada wacharukia ulaji wa Supu ya Pweza