Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Ilala inamshikilia Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa ‘Chama cha Kijamii’ CCK, Renatus Gregory Muabui kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali kutoka TAKUKURU na kuomba rushwa ya Sh.Mil 50,000,000.
Inadaiwa kiasi hicho ameomba toka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya BECCO iliyopo Vingunguti Ilala DSM.
“Mtuhumiwa alikamatwa Desemba 10, 2019 majira ya jioni katika Ofisi za BECCO akiwa amepokea fedha za mtego wa rushwa Sh.Mil 1 akiwa na dhumuni la kumsaidia Manraj Bharya katika tuhuma zake zilizokuwa zinamkabili Independent Power Tanzania Limited IPTL,” amesema Mkuu wa TAKUKURU Ilala, Christopher Myava.