Ni headline baada ya headlines kuhusu ugonjwa wa kipindupindu taarifa iliyonifikia ni kwamba sasa hivi upo mkoani Mwanza jimbo la Buchosa wilaya ya Sengerema.
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga mkuu wa mkoani hapo alisema..’Sasa hivi tatizo lipo Sengerema Jimbo la Buchosa kwenye kijiji cha Kanyara, wagonjwa wamelazwa katika Zahanati ya Lushamba… wagonjwa wengi wanatokea katika kijiji cha Kanyara kilichopo karibu sana na kisiwa cha Nkome,m Geita ambako tayari ugonjwa huo ulikuwepo, kwa hiyo katika muingiliano ukaleta tatizo‘-Dr James Kengia
‘Kwa takwimu nilizozipokea mpaka Octoba 13, 2015 idadi inafikia 26 katika wilaya ya Sengerema na wengine 104 walikuwa Skewere na mmoja alihudumiwa hospitali ya mkoa ya Sekou Toure Mwanza na mwingine alihudumiwa kwenye kituo cha huduma mashuleni lakini wote wameruhusiwa kwa halmashauri ya Jiji jumla yake ndio hao wamepata matatazo‘- Dr James Kengia
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBEIN wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.