Kituo cha Wanahabari watetezi wa Rasilimali na taarifa (MECIRA) kimeitaka serikali kuchukua hatua madhubuti za haraka na dharura ili kunusuru maisha ya wananchi jamii ya kimasai wanaoishi katika tarafa ya Ngorongoro iliyopo ndani ya hifadhi ya Ngorongoro sambamba na kunusuru mazingira na uhifadhi wa eneo hilo unaoonekana kuathiriwa kutokana na muingiliano wa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza.
Makamu Mwenyekiti wa kituo hicho mwanahabari mkongwe Maulid Kitenge ameyasema hayo kwa niaba MECIRA muda mfupi baada ya kamati tendaji ya taasisi hiyo kutembelea hifadhi hiyo kujionea utalii na maisha ya wananchi husika kuzingatia ukweli kuwa hifadhi ya Ngorongoro ndio hifadhi pekee nchini inayohusisha maisha ya binaadamu, mifugo na wanyama
Miongoni mwa mambo yaliyomsikitisha Kitenge ni jinsi wakazi wa maeneo hayo wanavyoishi kwa kukosa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo maji, barabara, Hospital n.k
Kitenge ameishauri Serikali kuwatafutia mahali salama pakuishi kwakazi waliopo hifadhini ili wapate huduma umuhimu za kijamii na waweze kuendelea kama binadamu wengine.
Nae Mjumbe MECIRA Oscar Oscar ameshangazwa baada ya kutembea umbali zaidi ya Km 45 lakini hajaona Wanyama zaidi ya pundamila kuchanganyika na mbuzi, ng’ombe kitendo ambacho kinahatarisha afya za wanyapori na usalama wao,
Pia ameogopeshwa na kasi ya ongezeko la wanyama wa kufugwa ng’ombr mbuzi kitu kinachosababisha Wanyamapori kukimbia, na kugombania malisho