Bado Taifa lipo kwenye siku 21 za maombolezo ya kuondokewa na aliekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, leo tumefika Shule ya Sekondari Sengerema ambapo Hayati Magufuli aliwahi kufundisha masomo ya Chemistry na Hesabu enzi za uhai wake, hapa tumeoneshwa kiti alichokitumia wakati akiwa Mwalimu Shuleni hapo (1982) .
“Hiki kiti kina miaka karibu (40) ndo kilitumika wakati ule Hayati Dkt. Magufuli akiwa ofisini kwake Idara ya Kemia, tumeendelea kuvitunza vitu hivi kama tulivyovikuta tungeomba Serikali ivitunze vitu hivi kama kumbukumbu kwenye Makumbusho ili vizazi vije kuona yaliyofanywa na Hayati Magufuli mengi katika Taifa hili”———Mkuu wa Idara ya Chemistry