Watu wengi tumezoea pale unapotokea msiba kutoa maneno yanayoonesha kuhuzunika na hata kutamani marehemu arudi. Hii ni tofauti kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambapo January 21, 2018 ameondokewa na mama yake mzazi Ruth Basondole Gwajima.
Kupitia kurasa zake za Mitandao ya kijamii Gwajima amesema mama yake mzazi amefariki akiwa na umri wa miaka 84 na mazishi ya mama yake yatafanyika January 25, 2018 Salasala jijini Dar es Salaama.
“Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni. Kuna Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu.” -Gwajima
MSIBA WCB: CHANZO CHA VIFO VYA MASHABIKI WAWILI WA WCB KWA MPIGO