Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya stori iliyoripotiwa ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Muuaji msikitini awaponyoka polisi’
#NIPASHE Muuaji msikitini Mwanza amewatoroka polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake pic.twitter.com/L3AV8U4bba
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
Gazeti hilo limeripoti kuwa jeshi la polisi mkoani Mwanza limesema mtuhumiwa wa ujambazi waliyemkamata kwa matukio mbalimbali ya uhalifu yakiwamo ya uporaji maduka ya miamala ya kifedha na mauaji ya watu watatu msikitini, Hamis Juma, ametoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi wakati akiwapeleka mlimani kuwaonyesha wahalifu wenzake.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Ahmed Msangi alisema juzi mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa Nyegezi, alikuwa mikononi mwa polisi akiwapeleka walipojificha wenzake katika mlima Kiloleli Nyasaka kata ya Kirumba wilayani Ilemela.
Msangi alisema baada ya polisi na mtuhumiwa huyo wa ujambazi kufika eneo la tukio saa 8:00 usiku ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima huo walianza kurusha risasi kwa askari ambao walitaharuki na kujibu mashambulizi huku wakimsahau mtuhumiwa aliyewapeleka ndipo alipopata mwanya wa kutoroka.
Aidha alisema katika mapigano hayo, polisi walikamata bunduki aina ya shortgun iliyokatwa mtutu na kitako na risasi moja kwenye chemba iliyotupwa na majambazi hao.
Unaweza kuzipitia hapa habari nyingine kubwa kwenye magazeti ya July 05 2016
#MWANANCHI TRA imesema mwananchi atakayetozwa gharama ya ziada na benki tofauti na ilivyokuwa awali, atoe taarifa pic.twitter.com/E8BD9pGpw6
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE Ukali wa Rais Magufuli ktk suala la ulipaji kodi kumesababisha wafanyabiashara kufurika kulipia leseni zao pic.twitter.com/iK2JC02vVz
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE Kitwanga afunguka juu ya kutimuliwa kwake kwa tuhuma za ulevi kwa kudai kuwa amesingiziwa, pic.twitter.com/minYHyanSj
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE CUF imewataka polisi kuwapandisha mahakamani viongozi wake wanaowashikilia kwa tuhuma za uchochezi Pemba pic.twitter.com/xm22FjQN1d
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE Taasisi ya maridhiano kuwasilisha ujumbe kwa Spika kuomba kuyakutanisha makundi mawili yanayosigana bungeni pic.twitter.com/kSDfZ99CP9
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE Lugola anayekabiliwa na shtaka la kuomba rushwa ya mil 30 alalamikia Jamhuri kuchelewesha kusikiliza kesi pic.twitter.com/fQoiaQf2Gj
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#NIPASHE Kisutu yawaonya Mdee, Waitara kwa kushindwa kufika kusikiliza kesi yao ya kumjeruhi katibu tawala mkoa pic.twitter.com/bczjxIha2U
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MWANANCHI Zikiwa zimebaki siku 18 mkutano mkuu CCM, hofu imetanda kwa wajumbe juu ya JPM kukabidhiwa chama hicho pic.twitter.com/ENrCjIx2rd
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MWANANCHI Kitwanga aacha pombe, asema Rais Magufuli ni mvumilivu na mwenye busara hivyo hawezi kuhoji uamuzi wake pic.twitter.com/mJB5RUkzVY
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MWANANCHI RC Makonda amewataka wakuu wa Wilaya Dar kufunga maeneo yote yanayouza shisha ndani ya wiki moja pic.twitter.com/xsOVFsaaFU
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MWANANCHI Mamia ya watu wameandamana Kenya kupinga mauaji ya kiholela yanayodaiwa kutekelezwa na maofisa wa usalama pic.twitter.com/S788oSlUPy
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MWANANCHI FBI wamhoji Hillary utumiaji wa barua pepe binafsi kwa matumizi ya Serikali akiwa waziri mambo ya nje pic.twitter.com/hWwkk5GasP
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MAJIRA Kitwanga aweka wazi ya Lugumi, asema hahusiki na kampuni hiyo, adai wauza unga wamehusika kumng'oa uwaziri pic.twitter.com/gPbee4TcAL
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#JamboLEO Watu 29 wamekufa ktk ajali ya mabasi mawili ya Kampuni ya City Boys yaliyogongana uso kwa uso Singida pic.twitter.com/zxl1cGUNm7
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#JamboLEO IGP Mangu amepata kigugumizi kueleza kama jeshi lake litaruhusu mkutano maalumu wa CCM, kufanyika ama la pic.twitter.com/qeML5MsVpz
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
#MTANZANIA Waziri Mkuu, Majaliwa apiga marufuku uvutaji wa shisha nchini na kulitaka jeshi la polisi kufuatilia pic.twitter.com/3ZnNoUJ7UU
— millardayo (@millardayo) July 5, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA JULY 5 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI