Umoja wa mataifa ‘UN’ umetoa ripoti ya mwaka 2017 kuhusu nchi zenye furaha zaidi duniani ikiwa ni muendelezo wa tafiti mbalimbali zinazofanywa kila mwaka
Unaambiwa ili nchi iweze kuingia katika list hii ni lazima ikidhi vigezo kama upatikanaji wa huduma za kijamii kwa urahisi kama vile elimu bure, afya bora, miundombinu, sehemu nzuri za kutembelea na amani.
1. Denmark
Denmark inatajwa kama nchi namba moja yenye furaha zaidi duniani ambapo moja ya sifa za nchi hiyo ni pamoja na kuwa na sehemu nzuri za kutembelea ambazo hufanya watalii wengi kutembelea, afya bora ambapo wananchi hupata huduma za afya bure, elimu bure pamoja na kupewa likizo ya mwaka mmoja kwa mama wajawazito.
2. Switzerland
Kuwepo kwa huduma muhimu za kijaamii kwa wananchi kumeiweka Switzerland katika nafasi ya pili ya nchi zenye furaha zaidi duniani.
3. Iceland
Hadi kufikia karne ya 20 Iceland ilikuwa moja ya nchi maskini zaidi Ulaya na kufikia 2013 ilikuwa katika nafasi ya 13 ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Kukua kwa uchumi wa nchi kuliifanya serikali kuwa na uwezo wa kuwekeza kwenye vitu vya muhimu kwa wananchi wake.
4. Norway
Norway ni moja kati ya nchi zenye idadi ndogo sana ya watu na rasilimali nyingi inazotosheleza watu wote. Hii imeifanya Norway kushika nafasi ya nne ya nchi zanye furah zaidi duniani.
5. Finland
Kwa mujibu wa ripoti ya UN Finland imetajwa kama nchi ya 5 katika list ya nche zenye furaha zaidi duniani.
6. Canada
Licha ya kuwa nchi ya pili kwa ukubwa duniani pia Canada imetajwa kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mwaka 2017.
7. The Netherlands
Licha ya kuwa ni nchi yenye idadi kubwa ya watu ukiziacha Bangladesh na China Netherlands pia ni nchi ya pili kwa kuzalisha mazao mengi ya biashara duniani. Hii imesaidia serikali ya Netherlands kutoa huduma za kijamii kama elimu na afya bure.
8. New Zealand
Ni moja kati ya nchi zinazosifika kwa ufugaji wa Kondoo wanaoiletea nchi hiyo maendeleo makubwa na kuifanya serikali iweze kuwekeza kwenye mwendeleo ya kijamii.
9. Australia
Australia imetajwa kuwa ni nchi namba 9 kwa kuwa na furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti ya UN 2017.
10. Sweden
Licha ya kushuka daraja kutoka namba 8 mwaka 2016 Sweden imebaki kwenye top ten ya nchi zenye wananchi wenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa UN 2017.
VIDEO: Waliozaliwa baada ya 1990 wana hatari ya kupata kansa ya utumbo, Bonyeza play hapa chni kutazama