Kanisa la Kiinjili la KKKT limeikumbusha jamii wajibu wa kuwajali na kuwaheshimu Wauguzi, Wakunga na Madaktari kwa kuwa ni kiungo muhimu cha maisha yao kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza zaidi hamasa katika utendaji kazi wao.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomoni Masangwa, ametoa rai hiyo katika ibada maalumu ya kuombea wahudumu wa afya pamoja na ufunguzi wa wodi mpya za Hopsitali ya Seliani Ngaramtoni Jijini Arusha, Hospitali ambayo imekuwa ikihudumia watu wengi waishio pembezoni hasa jamii ya kifugaji.