Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo kikuu cha DSM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema ili nchi iweze kuendelea na kuwa na uchumi mzuri ni lazima iwe na watafiti wenye uwezo wa kugundua vitu mbalimbali vitakavyo iwezesha Serikali kutatua changamoto za wananchi wake bila kutegemea nchi nyengine.
Kikwete ameyasema hayo wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti na Mafunzo ya Ufugaji Samaki Wilayani Pangani kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha DSM na kujionea namna kinavyofanya kazi.