Siku moja baada ya mwenyekiti wa klabu ya Yanga ambaye amechukua fomu ya kuomba nafasi hiyo ya uenyekiti wa klabu hiyo kwa mara nyingine Yusuph Manji kumtuhumu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Aloyce Komba kupanga hujuma dhidi yake, Komba ambaye ni mwanasheria ametangaza maamuzi mapya June 3 2016.
Komba ambaye alitajwa katika audio clip ya watu wa pembeni wanaopanga kutaka kumuhujumu Manji kwa kumshawishi yeye kwa fedha ili akate jina la Manji, ametangaza kujitoa nafasi ya uenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga kutokana na Manji kukosa imani nae, hivyo yeye hatojihusisha na lolote lile kuhusu uchaguzi wa Yanga.
“Ndugu waandishi mimi wakili Aloyce Komba ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF nimeamua leo June 3, kujitoa kusimamia uchaguzi wa Yanga, kwa sababu zifuatazo kwanaza nimetuhumiwa kupanga njama za kumuhujumu Yusuph Manji, hivyo siwezi kuendelea kusimamia uchaguzi ambao watu hawana imani na mimi”
KAMA ULIIKOSA VIDEO YA MANJI AKITAJA WANAOHUJUMU UCHAGUZI WA YANGA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE