Baada ya rapper Nicki Minaj kumtambulisha mpenzi wake mpya Kenny Petty ambaye anahusishwa na tuhuma za ubakaji pamoja na mauaji watu wengi waliongea vitu vingi vibaya kuhusiana na mwanaume huyo na kumpa majina mbalimbali.
Nick Minaj amemtishia Mtangazaji Jesse Palmer wa kituo cha Daily Mail TV kuwa atampeleka Mahakamani hii ni kutokana na kuongea kitu ambacho kimemchafua na kumkera Rapper huyo, pia amemtaka Mtangazaji huyo atafute Mwanasheria mapema.
Nicki Minaj ameyaandika hayo kupitia ukurasa wake wa instagram “Ni bora upate Mwanasheria mzuri, Jesse Palmer umezungumza uongo kuhusu mimi kwenye TV na sasa nakushtaki , ni bora ukaweza kujitetea ulichokisema kuhusu mimi na kwa ushahidi”
EXCLUSIVE: HAMISA AMEJIBU KWENDA DUKANI KWA WEMA NA KUHUSU OFFICIAL LYYN