Baada ya msanii Maua Sama pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown kukamatwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wameenda kinyume na sheria za Benki Kuu kwa kuchezea hela ya Tanzania.
Mchekeshaji Idris Sultan ni miongoni mwa wasanii walioguswa na hiki kinachoendelea kati yao na kuamua kumtetea Maua Sama na kusema kuwa Maua Sama hakuwa na lengo la kuivunjia heshima fedha yetu na benki kuu kwa ujumla ila inatupasa tujue lengo.
Idris Sultan aliongezea na kusema kuwa angeishauri serikali imtumie Maua kuelimisha wengine kupitia adhabu aliyoipata mpaka sasa na kuamini kuwa lengo sio kukomoana wala kuonyeshana nani zaidi lengo ni kutunza vyetu wenyewe.
“Binafsi ningependa kumuombea msamaha Maua kwakuwa lengo sio kuivunjia heshima fedha yetu na benki kuu kwa ujumla. Katika harakati za kujitafutia ugali makosa yatafanyika tu ila muhimu ni tukae tukumbuke lengo”
“Lengo sio kukomoana, lengo sio kuonyeshana nani anajua zaidi, lengo sio kuwekeana mabavu bali lengo ni kuelimisha jinsi ya kutunza vyetu wenyewe”
“Ningependa ku-propose mumtumie Maua kuelimisha wengine kupitia influence yake na adhabu aliyopata mpaka sasa tufanye imetosha. Hakuna aliye juu ya sheria ila tuvae tu uhusika wa lengo”
S2kizzy kazungumza Luffa kufukuzwa Wanene “Luffa kasepa, anamiliki studio”