Kupitia mahojiano aliyoyafanya Rapper Meek Mill na kituo cha Radio cha Real 92.3 ametoa ushauri kwa Rapper Tekashi ambaye yupo jela kwa sasa akisubiri Hukumu ya makosa ya kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.
Meek Mill amekuwa mtu wa pili kutoa ushauri kwa Tekashi baada ya The Game, rapper huyo alisema kuwa Tekashi ni kijana mzuri lakini anapaswa kupunguza matendo ya kihuni hasa wakati huu anapopitia umaarufu na hadhani kama aliongoza kundi hilo.
“Najua unafanya hivi ili kupata hela lakini inabidi upunguze kwasababu unakosana na watu wengi sana , kuna siku nilikutana na Tekashi na sikutaka kuzungumza nae kuhusu maisha ya jela nilitamani kumwambia unapata hela sasa hivi huwezi kuishi kama unavyoishi sasa hivi”
“Kutokana na maisha ya jela anayoyapitia najua watu hawaamini kama alifanya makosa yale hii ni kutokana na kundi lilikouwa likimzunguka na sidhani kama aliongoza kundi hilo nadhani ni kijana mzuri”
https://youtu.be/FAMjpFXyqMQ
EXCLUSIVE: AY kafunguka mengine usiyoyajua kuhusu Nyumba na Uraia wa Marekani