June 2 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli wakati akizungumza na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa alizungumzia juu ya uhujumu wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na kuagiza watu hao kushughulikiwa ipasavyo.
Baada ya agizo hilo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi leo amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tatizo la uhujumu wa miundombinu hiyo na ameitoa hii taarifa…….
>>>”katika kipindi cha siku mbili watu 49 wamekamatwa na polisi wilayani Kinondoni wakiwemo wamiliki wa magari, bajaji na bodaboda kwa makosa ya kuingilia miundombinu ya Mwendokasi kinyume cha sheria. Kati yao watuhumiwa 43 watapelekwa mahakamani siku ya jumatatu hali inaowafanya kuyatumia mapumziko ya Juma wakiwa mahabusu“
Mkuu wa Wilaya ameagiza Polisi wilayani Kinondoni kuendelea na zoezi la kuwakamata wale wote wanaogeuza vivuko vya barabara za DART kuwa sehemu za kulala na kujisaidia.
“Tumewaagiza Polisi kuwakamata wote wanaolala na kujisaidia kwenye vivuko vya barabara hata wale ambao wamesimama kule juu saa za usiku bila kazi yoyote wakamatwe na washitakiwe kwa sheria za uzembe na uzururaji, wengine hawa ni vibaka na wengine ndio wanaolala na kujisaidia huko usiku.“
ULIIKOSA HII AJALI YA BASI LA HARAKA NA PIKIPIKI ILIYOTEKEA DAR MAY 19 2016 NA KUUA MMOJA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE