Maafisa wa kiusalama jijini Mombasa wamefanikiwa kukamata shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin,mkuu wa kikosi cha kupambana na mihadarati Hamis Masha amesema kwamba shehena hiyo lenye kilo 341.7 ambayo thamani yake nishilingi bilioni 1.1.
Shehena hiyo imenaswa baada ya msako wa siku kadhaa unaoendelea Kenya dhidi ya meli ya MV Bushehr Amin Darya ambayo haijulikana imetoka nchi gani.
Kwa sasa maafisa wakuu wanajaribu kufatilia ushahidi walio nao ili kujua chanzo na sehemu ilikokuwa ikipelekwa mihadarati hiyo iliyo naswa Jioni ya July 15 baada ya meli hiyo kuweka nanga bandari ya Mombasa.
Wiki uliopita washtakiwa wawili walikamatwa baada ya kunaswa na pakiti ya kilo moja ya dawa aina Heroin na uchunguzi ulipowafatilia zaidi wachunguzi hao walipata kilo 341.7.